Huu ni mwezi wa ngapi?

Sasa nawaletea kitendawili rahisi alichokitunga mtaalam maarufu wa vitendawili, yaani Martin Gardner. Nimekibadilisha kidogo kwa ajili yenu.

Swali ni rahisi tu: ni mwezi gani unaoashiriwa na alama zisizo za kawaida zilizopo kwenye mchoro?

Ukipata jibu, unaweza kujaza fomu hapo chini. Nitatangaza majina ya walioweza, lakini tuzo ni sifa tu.