Maneno (na maeneo) yanayojichanganya

Ni mchezo wa kiubunifu unaokiumiza sana kichwa. Ila, ukipatia majibu … hadi raha!

Nimekupa herufi ya kwanza ya kila neno, na majibu yote ni maeneo ya Tanzania – mengine ni miji, mengine ni mengine.

Nasisitiza pia kwa mara nyingine ubunifu katika matumizi ya maneno na hata herufi. Kwa mfano, nawaonyesha namna kupata jibu la “Bila kuiba Stoney (5) – T…“:

  • Stoney ni aina ya soda lenye jina lingine, yaani “tangawizi”.
  • “Bila kuiba”, maana yake hapa ni kuondoa “wizi” kwenye jibu.
  • Hivyo, jibu ni¬†Tangawizi bila wizi, yaani “Tanga”

Maeneo mengine nakuachia. Kazi ni kwako – kila la heri!

Kama ungependa ku-download au kuchapisha, bonyeza hapa kupata pdf.

Majibu yatabadilika rangi ukipata neno nzima sahihi. Na majibu yote nitayaweka hapa mwisho wa mwezi huu (Januari 2017).

Kama ungependa tuzo (sifa tu!) ya kutajwa jina kwamba umeyaweza maneno yote, jaza majibu hapa.