Je, ungetumia dakika ngapi kuvuka daraja hili?

Watu wanne – Remmy, Koffi, Miriam na Oliver – wapo upande mmoja wa mto. Kuna daraja, lakini si imara sana, haliwezi likabeba zaidi ya watu wawili kwa wakati. Ni usiku wa manane, na hakuna anayeweza kuvuka bila kutumia tochi. Ila, wana tochi moja tu, na mto ni mpana, kiasi kwamba hawawezi kurusha tochi kutoka upande mmoja hadi mwingine, lazima ibebwe.

Remmy anatumia dakika moja kila akivuka daraja. Koffi anatumia mbili, Miriam anatumia tano na Oliver anatumia dakika kumi. Ikiwa wawili wanatembea kwa pamoja, lazima watumie mwendo wa anayetembea taratibu zaidi.

Je, ni dakika ngapi wanazozihitaji ili wote wanne waweze kuvuka salama?

Toa jibu lako hapo chini, nitatangaza washindi mwisho wa mwezi huu (Januari 2017). Usipate matumaini mengi lakini, kwa vile tuzo ni sifa tu!


Chanzo: Alex BellosCan you solve my problems?