Sayari ya maneno

Je, unaweza kutengeneza sentensi kamili (ya Kiswahili) kwa kutumia herufi zilizopo kwenye sayari hapo chini? Lazima uanze na “H” iliyopo chini kabisa ya sayari, na utumie njia inayopitia kila herufi bila kurudia na bila kuvuka mstari hata mmoja. Pia, unatakiwa kumaliza na herufi inayokurudisha ulipoanza.

 

Kitendawili hiki kiliwahi kuchapishwa katika gazeti moja maarufu nchini Merekani, takribani miaka mia iliyopita. Mwandishi alikaribisha wasomaji kumtumia majibu yao kwa barua, akapata majibu mengi yaliyosema hakuna njia inayowezekana.

Vipi, wewe unasemaje? Njia ipo? Toa jibu lako hapa.

Jibu nitaliweka hapa mwisho wa mwezi huu (Januari), pamoja na majina ya walioshinda. Kama wapo. Tuzo ni sifa tu.

Kila la heri!


Chanzo: Alex BellosCan you solve my problems?

One comment

Comments are closed.